Michezo

Video: Masau Bwire atoa siri kutembea na rundo la simu

Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amezungumzia sababu za kutembea na simu zaidi ya saba nyakati zote anapoonekana.

Bwire ambaye ni miongoni mwa wasemaji wachache wa klabu za soka nchini wanaovutia pindi wanapofanyiwa mahojiano na vyombo vya habari amesema hupenda kutembea na simu zaidi ya saba.

“Nikweli leo kidogo zimepungua nyingine zipo kwenye begi zinachajiwa zinapata chaji kupitia ‘power bank’.” Masau Bwire ameyasema hayo kupitia Bongo5.

Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire

Masau Bwire ameongeza “Chanzo hasa cha mimi kuwa na simu nyingi ni ninyi wanahabari kilammoja anakuwa na mtandao wake sasa akipiga kwa mtandao fulani anakuambia huna huu sasa kama huna unakuwa ushamtia katika shida na mahojiano yake yanakuwa ya haraka haraka kwakuwa anahofia salio litakata.”

“Sasa nikaona ili kuondoa shida hii basi kilamtandao uwepo na uwe hewani kwahiyo hilo hasa ndiyosababu kubwa ambayo imenifamnya nilazimike kuwa na simu katika mitandao yote inayopatikana Tanzania.”

“Niko na mitandao yote ambayo inapatikana Tanzania ikohewani kwahiyo kilammoja akiwa nashida katika mtandao huo aweze kunipata na ninatembea nazo kwasababu muda wowote wanahabari huwa wananitafuta wananipigia kwa hiyo ninakuwa na simu muda wote wanapopiga basi wanipate hewani.”

Msemaji huyo nae vutia kumsikiliza katika mahojiano hasa pindi anapozungumzia timu yake ya Ruvu Shootingi amesema “katika mahojiano wapo ambao wanamtandao mmoja akinipigia huku akinikosa kwa bahati mbaya simu imezima chaji sasa hana maarifa na akili nyingine kujuwa kwamba huyu ana simu zisizopungua saba na anayo mitandao yote ngoja nijaribu mitandao mingine.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents