Tupo Nawe

Video: Mimi ndiye niliwashawishi SoundCity na MTV wawe na Top Ten za Afrika Mashariki – Diamond

Diamond Platnumz ana mchango mkubwa katika ukuaji wa muziki wa Afrika Mashariki kimataifa kutokana na jitihada anazozifanya akiwa kama msanii mwenye mafanikio Afrika, japo kuwa anasema huwa hapendi kutangaza kila anachokifanya.

diamond p

Wiki iliyopita Diamond alipokuwa akihojiwa na mshindi wa Tuzo Za Watu, D’Jaro Arungu wa TBC FM kwenye kipindi cha Papaso, alitaja baadhi ya mambo ambayo ameshiriki kufanya katika kuukuza muziki wa Afrika Mashariki.

Muimbaji huyo wa ‘Utanipenda’ amesema yeye ndiye aliwashawishi SoundCity Tv ya Nigeria kuanzisha kipindi cha Top Ten East ambacho huonesha chati ya video za wasanii wa Afrika mashariki, na kuongeza kuwa walizungumza pia na MTV Base kuanzisha kipindi kama hicho.

“Mimi na crew yangu yaani Wasafi ndio tulizungumza na SoundCity TV wakaweka kipindi cha Top Ten East, SoundCity ni Tv kubwa sana Nigeria, sisi tulizungumza na MTV wakaweka ile Top Ten ya East Afrika ipo pale MTV.” Alisema Diamond alipokuwa akizungumzia mchango wake kwenye muziki wa Tanzania na Afrika mashariki.

Tazama Interview yote hapo chini, ambayo pia alizungumzia kuhusu MTV kumshirikisha kutoa maoni kuhusu video za wasanii wa Tanzania zinazotumwa kwenye kituo hicho ili zipitishwe kuoneshwa.

https://youtu.be/1f2_Y1rp5Hw

https://youtu.be/QhFX1rfSHU8

https://youtu.be/Nlsmqy3rD6g

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW