Burudani

Video: Rama Dee azungumzia ukaribu wake na Lady Jaydee

RnB Star Bongo, Rama Dee amezungumzia ukaribu wake Lady Jaydee na kueleza kiwango cha urafiki wao kwa sasa ni sawa na ndugu.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Nibebe’, amesema Lady Jaydee ni rafiki wa kweli, halafu ni rafiki wa kawaida na kitu kingine anapenda changamoto.

“Ina maana akikosea unamwabia, na ukikosea anakuambia aisee umezingua, kwa hiyo inakuwa simple sana kuishi na yeye, nashangaa tu tumeshibana, tunaelewana, sehemu tulipokosea tunarekebishana. Urafiki wa namna hiyo sasa hivi umefikia kama ndugu yangu kwa sababu muda wote naweza nikampigia simu tukazungumza,” Rama Dee ameiambia Bongo5.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano kati ya Lady Jaydee na Spicy, alijibu kuwa “Sina experience sana, mimi nikikaa na Jide tunaongea tu mambo yetu ya muziki, maisha ya kawaida, hatujawahi kudi-discuss mtu binafsi au kum-discuss huyo Spicy, hatujawahi kufanya hivyo,” amesisitiza.

Rama Dee na Lady Dee wamewahi kutoa wimbo pamoja ‘Kama Huwezi’ uliotoka mwaka 2013. Tazama interview nzima hapa chini.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents