MichezoUncategorized

Video: Samatta kama kawaida awanyoosha Lech Poznan michuano ya Europa league

Mshambuliaji hatari wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta hapo jana aliiandikia bao la kwanza timu yake dhidi ya Lech Poznan mchezo uliyo malizika kwa jumla ya mabao 1 – 2.

https://www.instagram.com/p/BmjbNIbnYFp/?taken-by=samagoal77

Mchezo huo wa marudiano wa michuano ya Europa league umeshuhudia Samatta akiipatia bao la kuongoza KRC Genk ndani ya dakika 19 kipindi cha kwanza kisha Leandro Trossard akifunga la pili dakika 45+1 ndipo wenyeji Lech Poznan wakaamka na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 50 kupitia kwa mchezaji wao Tomasz Cywka.

Samatta afanya yake KRC Genk ikichomoza na ushindi dhidi ya Lech Poznan

Katika mchezo wa awali uliyopigwa nchini Ubelgiji, Samatta maarufu kama Samagoal alipachika bao kupitia mpira wa kichwa dakika ya 56 kipindi cha pili mechi ambayo ilimazika kwa kupata ushindi jumla ya mabao 2 – 0.

Related Articles

4 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents