Habari

Video: Sheikh Kishk atangaza rasmi kuanza kutumia mitandao ya kijamii

Sheikh mkubwa Afrika Mashariki na kati, Nurdeen Kiskh ameamua kuanza kutumia mitandao ya kijamii baada kupokea wito kwa kipindi kirefu kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu.

 

Kishk amesema watu wengi wamekuwa wakinufaika kwa kutumia jina lake katika mitandao ya kijamii.

“Kumekuwa na watu wakitumia jina langu katika mitandao ya kijamii na wapo wengine wamefikia hatua hata ya kutaka kunifungulia, nimekubali kuitika wito wao na kuufanyia kazi na hatimae sasa napatikana katika mitandao yote ya kijamii.”Amesema Sheikh Kiskh.

Sheikh, Nurdeen Kiskh

Sheikh Kiskh ameongeza “Habari njema zaidi kwa jamii nimeanzisha Tv inayoitwa Kishk Online Tv na inatambulika hivyo katika mtandao wa Youtube.”

“Kishk Online Tv hailengi jamii ya kiislam kwa sababu wanaonifatilia na kuniunga mkono wadau wangu kwa ujumla ni watu wajamii zote. Jamii itarajie kupata mambo mbalimbali yaliyo mazuri hasa kupata mawaidha ambayo ataweza kusikiliza hata mtu asiye na dini.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents