Michezo

Nguli wa kubashiri Madee aimezea mate Jackpot Ya SportPesa

Madee Ali ni miongoni mwa wasanii wa muziki wakongwe kabisa nchini huku pia akiwa ni mmoja kati ya wakurugenzi wa lebo ya muziki ya Tip Top Connection ambayo ni lebo iliyowatoa wasanii wakubwa nchini akiwemo Dogo Janja.

Madee akiwa na uzi wa Arsenal FC

Mbali na kuwa mwanamuziki mwenye mafanikio, Madee ana kitu cha ziada, kwani amekuwa ni mdau mkubwa wa michezo ya kubashiri.

Madee ni miongoni mwa wateja wakubwa wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa na mara kwa mara amekuwa akishinda pesa nyingi ambazo amekiri kuwa huwa zinamsaidia kuendesha maisha yake.

Akiwa mmoja wa wageni waalikwa wa SportPesa, Madee alichezesha droo ya kumpata mshindi wa 14 wa bajaji ya TVS KING ambapo siku hiyo alipatikana mshindi kutoka Kagera, Wilson Winchelslaus, 21.

Baada ya droo, mtangazaji wa shoo hiyo ya Shinda na SportPesa inayoruka Clouds TV kila siku kuanzia saa 1:20 usiku, Charles Gibebe alipata fursa ya kupiga stori mbili tatu na Mdee, na hivi ndivyo maongezi yalivyokuwa;

SP: Ulianza vipi kujihusisha na michezo ya kubashiri?

Madee: Mimi nilikuwa miongoni mwa watu wagumu kuamini katika masuala ya michezo ya kubashiri na mara ya kwanza michezo hii inaingia, nilikuwa naona washkaji zangu wanaenda kwenye vibanda na makaratasi, mimi nikasema siwezi kufanya hayo mambo, lakini nikawa naona kuna muda wanapata na muda mwingine wanakosa.

SP: Kwanini uliamua kuchagua SportPesa?

Madee: Kwa mara ya kwanza SportPesa inakuja nikawa nafuatilia na wana wakawa wananiambia kuwa SportPesa unaweza ukacheza ukiwa kitandani kwako na sehemu nyingine basi nikaona hii ndio sehemu ambayo mimi naweza nikacheza na nilipokuja kuamini ni siku moja ambayo mshkaji wangu anaitwa Regan aliposhinda Milioni 3 na akaniambia hela inaingia sasa hivi, na hapohapo hela ikaingia.

SP: Mara ya kwanza unashinda, ilikuwa kiasi gani?

Madee: Siku moja mwanangu alikuwa anadaiwa ada ya shule na mimi huwa sipendi kwenda benki kutoa hela nikamwambia mshkaji wangu akanishawishi tuweke ubashiri na ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza.

Ilikuwa ni siku ya UEFA nikashinda Milioni 1.2 nikakatwa VAT basi ikabaki Laki tisa, na nilikuwa nimeweka Sh 30,000/= tu kwa mechi sita na niliposhinda, nikachukua ile hela na kwenda kuilipa ada ya mwanangu na kuanzia pale ndio nikawa mfuasi mkubwa wa SportPesa.

SP: Kiasi kikubwa kushinda na SportPesa ilikuwa ni Sh ngapi?

Madee: Hela kubwa kushinda ilikuwa ni Sh Milioni 6 ambayo nilishinda wiki iliyopita tu kwa Sh 50,000 na niliweka mechi saba tu

SP: Umeridhika na kiasi unachoshinda au una mpango wa kupiga pesa nyingine ndefu zaidi ya hiyo?

Madee: Bado sijapata zile hela ninazozitaka zile zaidi ya milioni 200 za Jackpot lakini pia nashukuru Mungu kwani kupitia michezo hii nimepata marafiki ambao huwa tunashauriana, na kuwa na marafiki ni mafanikio tosha.

SP: Wewe ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Arsenal, Je, ukiwa unabashiri huwa unaipa Arsenal ushindi au unaiua?

Madee: Kuna mechi ambazo huwa nabashiri na kuna mechi ambazo nazipisha ili kuepuka maumivu mawili ya kufungwa na kukosa hela kwa pamoja.

SP: Unawaambia nini watanzania ambao bado wanasita sita kucheza na SportPesa?

Madee: Hao siwalaumu kwasababu ndivyo nilivyokuwa mimi mwanzoni lakini itafika muda wataona kuwa hivi vitu vipo kweli na sio vya kudanganya kwasababu unajua wabongo wameshaliwa sana kwenye michezo hii ya kubashiri lakini kwa SportPesa mimi nitakuwa shahidi namba moja.

SP: Una mpango wa kushinda Bajaji ya TVS KING kupitia promosheni ya “Shinda na SportPesa”?

Madee: Bajaji ni moja ya usafiri ambao umekuwa maarufu sana hasa hapa Dar kutokana na suala zima la foleni kwahiyo watu wanabashiri sana ili kujishindia za kwao na nawasikia marafiki zangu wanazizungumzia sana na mimi naendelea kuisaka ipo siku mtaniita mje kunipongeza hapa (kicheko)

Madee: Nguli Wa Michezo Ya Kubashiri Anayeimezea Mate Jackpot Ya SportPesa

Madee Ali ni miongoni mwa wasanii wa muziki wakongwe kabisa nchini huku pia akimiliki lebo ya muziki ya Tip Top Connection ambayo ni lebo iliyowatoa wasanii wakubwa nchini akiwemo Dogo Janja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents