Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Video: SportPesa wametupa ujanja wa nje ya uwanja – John Bocco

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na kikosi cha wekundu wa msimbazi,Simba SC, John Bocco ameeleza namna alivyofurahishwa kwa kufika katika ofisi za wadhamini wao ambao ni kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa na kutumia nafasi hiyo kujifunza vitu ambavyo alikuwa havifahamu kama mchezaji.

Bocco ameyasema hayo baada ya kuzungumza na Bongo5 katika ofisi za SportPesa.

“Kwanza ni furaha kubwa hatujawahi kufika pia imekuwa fursa kwetu kujifunza vitu vingi ambavyo tulikuwa hatuvijui kuhusu SportPesa na kubadilishana mawazo na wadhamini wetu.”Amesema  Bocco

 

Jonh Bocco ameongeza “Naamini vitu vingi tulikuwa hatuvijui ambapo leo tumeweza kujifunza kama unania na umeelewa nini kilichosemwa unaweza kujua ni kwa namna gani unaweza kujiendeleza nje ya uwanja.”

“Wazamini wetu wa SportPesa tunawashukuru kwa kuweza kutupa kitu kizuri ambacho ni darasa zuri kwetu kwa maisha yetu ya baadae.”

Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba SC msimu huu baada ya kumalizana na timu aliyoichezea kwa misimu 10 mfululizo Azam FC.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW