Michezo

Video: TFF yaja na mipango ya kufufua soka la ufukweni

Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’ kwa kushirikiana na kampuni ya Shadaka Sports Management limeandaa tamasha la mchezo wa soka la ufukweni ‘Beach Soccer’ linalotarajiwa kufanyika Octoba 14 mwaka huu.

Salum Madadi ambaye ni kiongozi wa TFF amesema kuwa tamasha hilo litakuwa na jumla ya timu 12 ambapo litaanza majira ya tano asubuhi mpaka saa 11 jioni.

“Baada ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’ kupata kamati mpya ya utendaji imeadhimia kuliamsha mchezo wa soka la ufukweni na wanatarajia kuanza ligi mwezi Januari.”Amesema Madadi.

Nae muakilishi wa kampuni ya Shadaka Sports Management, Edigar Kibwana amesema kuwa wameamua kushirikiana na TFF kuhamasisha wdau wa mchezo wa soka la ufukweni.

“Licha ya tamasha ambalo tutalifanya malengo makubwa ni kuukuza mchezo wa soka la ufukweni na kuufanya uwe mkubwa zaidi kwa baraka za TFF.”Amesema kibwana.

Kibwana  amesema “Kwa sasa TFF hawajaja na kalenda rasmi ya mashindano lakini tumeingia ubia katika kuandaa matamasha ya kutengeneza hamasa ya mchezo huo.”

“Tumejipanga kama kampuni katika kuhakikisha tunatafuta wadau kuja kuwekeza katika mchezo huu kwa maana ya taasisi na TFF kunufaika kwa pamoja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents