Michezo

Video: Utata wamalizwa kati ya gari la Formula 1, ndege ya kivita na pikipiki ya mashindano kuwa ipi yenye kasi zaidi

Mara kadhaa kumekuwa na maswali juu ya chombo gani cha usafiri kati ya hivi kina mbio zaidi ama spidi kali, gari la kawaida, gari la mashindano, ndege ya abiri, ndege ya kivita na pikipiki ya mashindano.

https://www.youtube.com/watch?v=9ftqgfdfznQ

Mapema mwishoni mwa juma lililopita madereva watano wakiwemo wawili wandege ‘pilots’, jijini Istanbul nchini Uturuki wameweza kututhibitishia kuwa ni chombo gani cha moto kati ya hivyo kina spidi zaidi kupitia tamasha la ‘Teknofest festival’.

Katika mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Istanbul imeshuhudiwa piki hiyo ya mashindano aina ya Kawasaki H2R ikiibuka kidedea kwa kuwa na spidi ya ajabu ambayo imetumia mita 400  pekee.

Hata hivyo kulikuwa na ushindani mkubwa katika hatua ya mwisho kati ya pikipiki hiyo dhidi ya Red Bull Formula 1 kabla ya bodaboda hiyo kukanya mstari wa ushindi wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na ndege ya kivita.

Dereva wa pikipiki hiyo aina ya Kawasaki H2R, Kenan Sofuoglu ameibuka mshindi baada ya kutumia robo tatu ya mile kwa sekunde 9.254.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents