Michezo

Video: Valencia akerwa na rafu aliyochezewa nahodha wa Tanzania, Morris Abraham 

Mchezaji wa Manchester United, Antonio Valencia ameonyesha hisia zake juu ya kitendo cha mchezaji wa timu ya taifa ya Burundi ya vijana U17 kumchezea rafu mbaya nahodha wa Tanzania, Morris Abraham kwenye mchezo wa kundi A, michuano ya kufuzu fainali za Africa kwa Vijana waliyo na umri chini ya miaka 17 (U17).

https://www.instagram.com/p/BmeFtG9hssk/?taken-by=antoniovalencia2525

Valencia ambaye ni beki wa United ameonyesha hisia hizo kwa kuposti kipande cha video kwenye mtandao wake wa Instagram kinachoonyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira uliyofanywa na Morris Abraham anayetumikia timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U17 ”Serengeti Boys” hadi kupelekea mchezaji huyo wa Burundi kumchezea rafu mbaya.

Watanzania wengi wametoa maoni mbalimbali kwenye Instagram ya Valencia baada ya kuiweka kipande hicho cha video huku tukio hilo likiwa limesambaa kwa wapenzi wengi wa soka duniani.

Valencia alisajiliwa kama winga mwaka 2009 na kujikuta akiwa bora zaidi kwenye safu ya ulinzi ambapo imempelekea kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu.

Kwenye mchezo huo wa kwanza wa kundi A, vijana wa Tanzania waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Burundi mabao yakifungwa na Kelvin John dakika ya 11, Agiri Ngoda akifunga dakika ya 29 wakati la Burundi likifungwa na Munaba Edson dakika ya 20.

Michuano hiyo ya kufuzu fainali za Africa kwa Vijana U17 yameanza siku ya Jumamosi Agosti 11 na kutarajiwa kufikia tamati yake Agosti 26,2018.

Related Articles

9 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents