Habari

Video za AY ‘Party Zone’ na ‘Money’ ndiyo video pekee za Tanzania zinazooneshwa na TV ya Ufaransa TRACE

CEO wa Unity Entertainment Ambwene Yessaya a.k.a AY ndiye msanii pekee wa Tanzania ambaye video zake zimefanikiwa kupenya na kukidhi viwango vya kuoneshwa na kituo cha TV cha kimataifa TRACE ya Ufaransa.

AY

AY amefunguka kupitia Daladala Beats ya Magic FM muda mfupi uliopita na kuzitaja ‘Party Zone’ na ‘Money’ kuwa ndiyo video pekee za msanii wa Tanzania zilizowahi kufanikiwa kuoneshwa na kituo hicho, hadi video mpya ya MwanaFA na yeye ‘Bila Kukunja Goti’ nayo kupitishwa hivi karibuni na kuongezeka kuwa ya tatu.

AY amesema Video zote zimefanyika Afrika Kusini na lengo la kuwekeza kiasi kikubwa kufanya video hizo nchini humo, ni kwa lengo la kufanya kazi za kiwango cha kuchezwa na vituo vikubwa kikiwemo Trace, Channel O, MTV Base na zingine.

Ameongeza kuwa licha ya video zake kupata heshima ya kuchezwa na kituo hicho lakini ‘Party Zone’ aliyomshirikisha producer wa MJ Records Marco Chali imewahi kushika nafasi ya kwanza katika chart za Trace.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents