Michezo

Vilio na machozi vyawatawala wachezaji wa Taifa Stars, matumaini ya AFCON 2015 yapotea rasmi

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana iliondolewa rasmi kwenye michuano ya kuwania kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kwa kufungwa mabao 2-1 na Msumbiji aka The Mambas.

IMG_9182
Mchezaji wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akilia kwa uchungu baada ya Stars kupoteza nafasi ya kucheza hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Afrika 2015.

Kichapo hicho kiliwafanya baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars akiwemo Shomari Kapombe kulia kama watoto wadogo.

“Taifa Stars imecheza mechi nyingi ambazo nimehudhuria, ndani na nje ya nchi. Sijaona wachezaji wakitokwa machozi kama Jana. Ndani ya chumba cha kubadilisha nguo niliona uchungu na machozi ya vijana wetu. Kwa pamoja walikuwa wanasema ‘nyumbani kama ugenini, ugenini ugenini’. Somo kubwa sana hilo,” ameandika Zitto Kabwe.

IMG_9173
Mbwana Samattah akishindwa kuzua kilio baada ya Taifa Stars kufungwa

Una maoni gani kuhusiana na kikosi cha Taifa Stars?

Picha: KiliLager.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents