Michezo

Wachezaji wa Bundesliga kufanyiwa uchunguzi wa ubongo, Shirikisho la Soka Ujerumani (DFB) lasema zoezi hilo ni lazima

Katika jitihada za kuzuia majeraha ya ubongo miongoni mwa wachezaji wa mpira wa miguu wa ligi ya Bundesliga, tume ya matibabu ya Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) imesema wachezaji wote wa daraja la kwanza na la pili watafanyiwa uchunguzi wa lazima wa ubongo kila mwaka.

Image result for heads goals in Bundesliga

Uchunguzi huo utakuwa sehemu ya ukaguzi wa afya wa kila mwaka na utaanza kutekelezwa msimu ujao, kwa mujibu wa toleo la Jumapili la gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag.

Christoph Kramer after his injury at the World Cup final in Brazil

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Ujerumani (DW ) Wataalamu wamekuwa wakionya kwa muda mrefu juu ya hatari za majeraha ya kichwa yanayotokana na mpira, ikiwa ni pamoja na pale mchezaji anaporuka juu ya mchezaji mwengine akijaribu kudaka mpira kwa kutumia kichwa.

Uchunguzi wa Uingereza uliochapishwa mnamo 2017 uligundua kuwa wachezaji wa mpira wa miguu wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupata majeraha ya ubongo, sawa na wanandondi au wachezaji wa soka ya Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents