Habari

Wakamatwa kwa kuiba mayai kutoka shamba la naibu rais wa Kenya

Wafanyakazi wanne wamekamatwa Kenya kwa kutuhumiwa kuiba mayai yenye thamani ya $25 kutoka shambani mwa naibu rais William Ruto, vyombo vya habari nchini vimenukuu maafisa wa polisi.

kuku

Kwa mujibu wa BBC, Uchunguzi umeidhinishwa baada ya msimamizi katika shamba hili lililopo huko Sugoi katika mkoa wa bonde la ufa kupiga ripoti kwamba kuna mayai yaliopotea, polisi inaeleza.

“Uchunguzi wetu wa awali umefichua kwamba wafanyakazi wanne wanaoishi ndani ya shamba hilo walihusika katika wizi huo lakini wote wamelikana hilo,” afisa wa polisi katika eneo hilo Zachariah Bittok amenukuliwa na vyombo vya habari nchini.

Inaarifiwa kwamba washukiwa hao wanaume wawili na wanawake wawili wanazuiwa katika kituo kimoja cha polisi katika enoe hilo ambako wanahojiwa.

Bitok ameliambia gazeti la The Standard kwamba msimamizi katika sehemu ya ufugaji kuku kwenye shamba hilo aligundua kwamba mayai yenye thamani ya shilingi 2,500 za Kenya yalipotea na ndio akaamua kuarifu maafisa wa polisi.

“Wafanyakazi wote wamekana kufahamu chochote kuhusu mayai hayo yaliopotea na meneja huyo akaanza kuyatafuta na kuwashutukia washukiwa hao wanne wakiwa wamezificha kreti hizo kwenye sehemu moja ya shamba, ,” afisa huyo ameeleza.

Taaifa hizo zimepokea kwa hisia tofuati nchini huku baadhi wakikejeli na kusema kwamba kuna mambo yalio muhimu zaidi kuangaziwa katika vyombo vya habari kuliko taarifa za kupotea kwa kreti 10 za mayai .

Wengine wakieleza kwamba kuna kila haki ya kuliripoti hilo maana ni haki ya mtu.

Baadhi wakipuuzilia mbali, na kulalamika kwamba ni kupoteza rasilmali nguvu za polisi.

Inaarifiwa washukiwa hao sasa watafikishwa mahakamani, na kreti hizo za mayai zilizopatikana zitatumika kama ithibati au ushahidi kotini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents