Michezo

Wakati tuna sajili wenzetu walikuwa wanawahi Airport na kubebana – Manara (+Video)

Msemaji wa Mabingwa wa tetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Haji Manara amesisitiza kuwa hawapo tayari kutolewa mapema kwenye michuano ya Caf Champions League na lengo lao bado lipo pale pale la kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.

“Target yetu ni Nusu Fainali, ndiyo lengo letu, inawezekana tusifikie lakini walau tukaribie angalau Robo Fainali.”- Manara

Haji Manara ameongeza “Hii ni simbasc na lazima tutimize kile ambacho Watanzani wanakiamini kuhusu hii klabu, hii ni klabu kubwa….. hatuwezi kutolewa mapema safari hii.”

Ikumbukwe kuwa Mnyama Simba msimu uliyopita walikuwa na lengo hilo hilo la kutinga hatua ya Nusu Fainali lakini liligonga Mwamba baada ya kutolewa hatua za mapema tu kitu ambacho wadau wengi wa mchezo wa soka nchini hawakukitarajia na hivyo kukamilisha ule msemo mpira ni dakika 90.

Kuangalia Video bofya HAPA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents