Habari

Wakazi kuzindua video mpya ya ‘Touch ‘ kesho (Nov 2), pia aelezea sababu za kuachia wimbo usio rasmi ‘Wanawake wa Dar’ (Audio)

Rapper Wakazi kesho Jumamosi (November 2) anatarajia kuzindua video ya wimbo wake ‘Touch‘ iliyofanyika nchini Afrika Kusini alipoenda kutumbuiza katika Big Brother The Chase. Lakini katika kuwaandaa mashabiki wake kuipokea video hiyo Wakazi ameamua kutoa wimbo wa freestyle ambao si rasmi unaoitwa ‘Wanawake wa Dar’.

wakazi

Wakazi ameuelezea wimbo wa ‘Wanawake wa Dar’ ambao unapatikana katika mixtape yake inayoitwa ‘I am Afrika Mixtape’ itakayotoka baadaye,

“Kusema kweli hii ngoma si kama ni rasmi kihivyo sababu ni kama freestyle zaidi inaitwa Wanawake wa dar, ni wimbo ambao Marekani uliimbwaga na Walle na unaitwa ‘Love Hate Thing’ kwahiyo mi nikaibadilisha na kuifanya Wanawake wa Dar, kwahiyo nimeiongea kwa hisia zangu jinsi navyoona mimi kimtazamo.” Alisema Wakazi

Pia rapper huyo ametoa sababu za kutoa ‘Wanawake wa Dar’ ilihali ‘Touch’ bado inafanya vizuri katika vituo vya radio kwasasa,

“halafu hiyo nimeifanya hivyo kwasababu siku ya Jumamosi nitakuwa nafanya uzinduzi wa video ya wimbo wa ‘Touch’ ambao ndio huo ambao redioni sasahivi unafanya vizuri, so natoa video yake rasmi siku ya Jumamosi so nikasema ngoja nitoe hii freestyle iwachanganshe watu kidogo kuelekea hiyo siku ya Jumamosi ambayo nitakuwa nafanya uzinduzi wa hiyo video.” Wakaza alizungumza kupitia Safari radio ya Mtwara jana.

Msikilize hapa
[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/118046546″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Sikiliza wimbo wake wa ‘Wanawake Wa Dar’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents