DStv Inogilee!

Wanafunzi wa kike waliokatisha masomo kwa kupata mimba au kukosa ada, kusomeshwa bure (+video)

Taasisi ya “Apps and Girls” hii ni taasisi inayochukua wanafunzi wa kike waliokatisha masomo kwa kupata aidha ujauzito au kukosa ada na kuwaendeleza wanafunzi hao kwa kuwapatia ujuzi zaidi kwenye masomo ya TEHAMA.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Machi 8, 2019 Mkurugenzi na Muanzilishi wa Taasisi hiyo, Caroline Kyarisiima amesema kuwa lengo kubwa la taasisi hiyo ni kumkomboa mwanamke kwani anaamini kuna wanawake wengi wanashindwa kufikia ndoto zao kwa sababu tu ya jinsia zao, ikiwemo kupata mimba wakiwa mashuleni.

Kwenye hafla hiyo, iliyoambatana na sherehe za maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani. Kulihudhuria pia na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Dkt. Inmi Patterson ambaye kwenye hotuba yake alikemea baadhi ya mila zinazodidimiza wanawake kimaendeleo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW