MichezoUncategorized

Wanaobashiri na SportPesa kujishindia safari ya kushuhudia EPL

Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini, SportPesa imetangaza kampeni yake mpya ambayo itawafanya wateja wake ambao wanabashiri mechi mbalimbali kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mechi ya EPL nchini Uingereza.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzanua, Abass Tarimba (katikati) akiwa katika uzinduzi huo.

Ukiachana na mamilioni wanayopata washindi kutokana na kupatia ubashiri wa mechi mbalimbali kupitia SportPesa, pia zile BET ID zitawapa ushindi mwingine wa kwenda Uingereza kushuhudia mechi za EPL.

Jumla ya washindi 8 watanufaika na dili hilo ambapo kila wiki mshindi mmoja atapatikana kupitia kampeni ya ‘Zali La Mwanaspoti’ inayoendeshwa na Gazeti la michezo la Mwanaspoti.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya Zali La MwanaSpoti

Wateja wanaobashiri na SportPesa wanatakiwa kununua Gazeti la Mwanaspoti na kujaza kuponi ambayo amepewaka katika gazezi la siku hiyo ambayo amebashiri.

Kuponi hiyo itahitaji mtu anayejaza awe ana BET ID aliyopewa baada ya kumaliza kubashiri mechi kupitia SportPesa huku BET ID ikiwa ni ile uliyobeti siku husika ambayo gazeti limengia mtaani.

Pia atatakiwa kujaza taarifa zake kamili pamoja na namba zake za simu na kicha kuipeleka kuponi hiyo kwa muuza magazeti.

Kwa maelezo zaidi tembelea katika mitandao ya kijamii ya SportPesa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents