Michezo

Wanaozungumzwa katika usajili barani Ulaya Jumatano hii, Raheem Sterling, Sergio Aguero na wengine

Manchester City imeanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa kimataifa wa England Raheem Sterling, 24. (Mirror)

Sterling

Mkufunzi wa Leipzig, Julian Nagelsmann na Jose Mourinho wanapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino, aliyefutwa kazi kama mkufunzi wa Tottenham. (Star)

Red Devils huenda wakalipa hadi £85m kumsaini mshambuliaji wa Salzburg na Norway mzaliwa wa Leeds-Erling Braut Haaland, 19. (Standard)Braut Haaland

Red Devils huenda wakalipa hadi £85m kumsaini mshambuliaji wa Salzburg Braut Haaland(kushoto)

Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Reading Danny Loader, 19, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, amepuuzilia mbali tetesi kuwa alitoa wito kwa Blues kutomsajili mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero kabla ahamie Manchester City. (Mirror)

Swansea na Stoke zinamtaka winga wa Celtic wa miaka 32- Jonny Hayes mkataba wake unapoelekea kukamilika. (Scottish Sun)Sergio Aguero

Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, amepuuzilia mbali tetesi kuwa alipinga usajili wa Sergio Aguero kabla ahamie Manchester City

Robert Moreno anatarajiwa kutoa kauli yake kuhusu hatma yake kama kocha wa Uhispania baada ya hatua ya mkataba wake kuvunjwa. (AS – in Spanish)

Wachezaji wa Manchester United wameombwa kutotoka nje kwa zaidi ya dakika kumi watakaposafiri kucheza na FC Astana katika ligi ya Europa kutokana na hali ya baridi kali nchini Kazakhstan. (ESPN)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents