Burudani

Wasanii 3 waliovaa sura za wasanii wengine

Kuiga kitu kizuri kutoka kwa mtu si dhambi ila kwenye muziki ukifanya hivyo sana unakuwa unaharibu ladha ya muziki wako hivyo hufanya watu kuweza kukuchoka mapema. Kuna baadhi ya sauti za wasanii huwezi kuzitofautisha kwenye nyimbo zao na sauti za wasanii wengine.

kopi

Chini ni baadhi yao:

Harmonize kwa Diamond

Hili si mara ya kwanza kulizungumza ila ukweli uliopo ni kuwa Hitmaker wa ‘Matatizo’ amekuwa akionekana kama Diamond namba mbili kutokana na style yake anayoitumia kwenye muziki kwa asilimia kubwa imekuwa ikiendana na ile ya bosi wake huyo.

Hivi karibuni mashabiki walionekana kuchoshwa na kitendo hicho lakini mwenyewe alikanusha kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika, “Mhhh copy! copy! copy!….. mwisho wa siku hata ukinya utaambiwa kunya kama weweusimcopy@diamondplatnumz ebwana mzee#simbaa video ijayo wacha nianze kuvaa Dera maana nguo zote ushazivaa #INDE in my BIO though .”

Kupitia wimbo wa ‘Bado’ unaweza kuthibitisha kile kinachosemwa na wengi.

Y Tony kwa Rich Mavoko

Ni muda mrefu nilikuwa nikifanya uchunguzi juu ya kile ninachokisikia kutoka kwenye nyimbo za Y Tony.

Nilianza kusikia kitu kama nilichowahi kukisikia kuanzia kwenye wimbo wa ‘Martina’ huku kwa mbali nikimsikia Rich Mavoko kumbe masikio yangu yalikuwa yananidanganya mpaka pale macho yalipomuona Y Tony.

Lakini kwa sasa ninaweza kuamini kuwa Hitmaker huyo wa Masebene ni kopi ya Mavoko kutokana na wimbo wake wa ‘Wivu Wangu’ aliouachia wiki iliyopita. Hakika ukiusikiliza wimbo huo unaweza Rich ndio kaimba tena unafanana na ule aliowahi kuuachia miaka miwili iliyopita ‘Silali’.

Desiigner kwa Future

Kwa hili lipo wazi kabisa kuwa rapper Desiigner ambaye yupo chini ya lebo ya G.O.O.D Music ya Kanye West anamkopi Future kutokana na style yake ya kurap.

Wimbo wa ‘Panda’ ndio ulimtambulisha rapper huyo huku baadhi ya mastaa wakubwa kama 50 Cent wakionekana kutomkubali kabisa msanii huyo. Hata hivyo Desiigner amewahi kukataa kumuiga Future.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents