Habari

Wananchi wamuumbua mkandarasi kwa kushindwa kukamilisha ujenzi ya daraja kwa miaka 5

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda imezidi kuwa mwiba kwa baadhi ya watu baada ya Wananchi wa Tabata Kinyerezi kumshtaki kwa mkuu wa mkoa mkandarasi wa kampuni ya Texas, Francis Musiba kwa kushindwa kukamilisha kwa wakati ujenzi wa daraja linaloonganisha Kinyerezi na Bonyokwa.

mkuu-wa-mkoa-wa-dar-es-salaam-paul-makonda-akiwa-katika-daraja-hilo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa katika daraja hilo

Wakizungumza kwa hasira mbele ya mkuu wa mkoa huyo katika ujenzi wa daraja hiyo, Wananchi hao wamesema daraja hilo ambalo nikionganishi muhumu cha wakazi wa Tabata Kinyerezi na Bunyokwa lilianza kujengwa miaka minne iliyopita.

“Mh Mkuu wa Mkoa tunaomba utusaide hili daraja likamilike, tumechoka na usumbufu ambao tunaupata. Hili daraja limenza kujengwa toka miaka minne iliyopita lakini mpaka leo hii halijakamilika,” alilalamika kijana mmoja.

Pia mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Swahumu, amesema daraja hilo limekuwa likisababisha hadha kubwa kwenye suala la usafiri kwani hakuna gari linaloweza kupita katika daraja hilo.

Hatua hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kumtaka mkandarasi wa mradi huo kueleza ni kwanini daraja hilo limechelewa kukamilika kwa wakati na kusababisha hadha kubwa ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.

“Kwanza sio kweli kwamba hili daraja limejengwa kwa miaka minne,” alisema Mkandarasi. “Hili daraja limeletwa hapa mwezi machi mwaka huu, lilikuwa lije hapa toka Novemba mwaka jana lakini Tanroad na Halmashauri walichelewa kukubalina na kulileta,”

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alimpatia siku 25 mkandarasi huyo awe amekamilisha ujenzi ya daraja hilo huku akimtaka Mkandarasi wa Halmashauri ya Ilala, Nyamagalula Masatu kuunda timu ya wataalamu ili kukagua ubora wa mradi huo.

“Wewe mkandarasi nataka mpaka tarehe 25 Disemba hili dajara liwe limekamilika, leo ni tarehe 24,  ukishindwa kukamilisha ndani ya muda huo basi hautapata tena kazi ndani ya Dar es salaam. Pia Mkandarasi wa Halmashauri ya Ilala unatakiwa kuunda timu ya wataalamu ili kukagua ubora wa hili daraja kwa sababu wakati nipo hapo juu daraja lilikuwa linatikisikila.” alisema Makonda

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents