Burudani

Wastara: Nikiingia bungeni, nitawatetea walemavu wenzangu

Msanii wa filamu, Wastara Juma ametangaza nia ya kugombea ubunge na amedai kuwa kipaumbele chake akipewa dhamana hiyo ni kutetea haki za walemavu ambao anadai wamesahaulika.

11424576_1611143409163873_1934672109_n

Wastara amefafanua zaidi azma yake kwenye Instagram:

Leo hii ni aibu zinajengwa barabara lakini hazima sehemu ya kupita walemavu, Leo hii ni aibu kuona shule nyingi za ulemavu. kwanza ni za zamani halafu hakuna hata vifaa vinavyoendana na dunia ya kisasa ya sayansi na teknolojia.

Ni aibu kuona hatuna viwanja vya michezo kwa walemavu wakati na sisi tunahaki ya kushiriki hata mashindano ya Paralimpic. Nimejaribu kuonyesha na kuwapigania walemavu wenzangu kupitia sanaa lakini nimeona sauti yangu ni ndogo na haisikiki kokote sasa nimeamua kuingia kwenye siasa ili nisamame na kuwapigania Walemavu wenzangu wasio na sauti nao sawa na kuona machozi, maumivu na mateso yao nayafuta vipi na pia ili niweze kufuta kiapo nilichoweka kwenye nafsi yangu baada ya kuona tunapokelewa vibaya ndani ya nchi yetu wenyewe kwamba lazima siku moja nitawapa furaha walemavu wenzangu kabla sijafa nitapigania haki zao za msingi ili nao au tujione tuna haki sawa na wengine nimekaa na dukuduku hili ndani ya miaka 5 sasa.

Huu ni wakati wa kulitoa na kujitoa kwa nguvu zangu zote kuhakikisha walemavu wanawekwa katika mazingira mazuri kama nchi za wenzetu waishi vizuri na kufikia hata nusu yake tu basi nitakuwa nimefikia lengo la kutetea haki za msingi kwa walemavu wenzangu sababu hata mim ni muhanga nimetumia lugha nyepesi ili nieleweke sina tamaa ya chchote ila sitakuwa sawa kufa bila kuwaweka wenzangu kwenye maisha ya haki na sehemu sahihi kwa sasa kuonyesha nilichohahidi moyo wangu ni bungeni najua kma si wew uliyelamaa basi ndugu rafiki jirani yako lazima atakuwa kwenye hali hii hivyo watanzania kutumia nguvu zetu kunisuport amtapoteza kitu bali mtaongeza msaada kwa wale wasijioweza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents