Burudani

Watanzania washindwa kutamba kwenye Nokia Don’t Break The Beat


Weekend iliyopita marapper wawili wa Tanzania walishindwa kutamba kwenye fainali za shindano la Nokia Don’t Break The Beat lililofanyika jijini Nairobi,Kenya.

Tanzania iliwakilishwa na Ally Abdallah Chuma pamoja na na Njama George Mtandika.
Rapper wa Kenya, X-Calibur Shahidi (Richmond Sangara) ndiye aliyevikwa taji la mshindi wa Nokia Don’t Break The Beat.
X-Calibur alimshinda mkenya mwenzie Kevin Otieno aka Ojiji, aliyeshika nafasi ya pili.

Hata hivyo mashabiki walichukia uamuzi huo kwakuwa wengi walikuwa wakimkubali zaidi Ojiji.
Baada ya kutangazwa kuwa Ojiji ameshika nafasi ya pili watu waliokuwa wamehudhuria fainali hizo walianza kuwazomea majaji.
Uganda iliwakilishwa na Kkeeya Nicholas na Sebbowa Kizito.

Fainali hizo zilipambwa na show ya wakali kama STL, Madtraxx, Keko na Mwana Fa

Mshindi amejinyakulia shilingi milioni tano za Tanzania pamoja na record deal ya mwaka mmoja chini ya Decimal Records.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents