Habari

Muigizaji Michael Clarke Duncan afariki dunia


Muigizaji wa filamu nchini Marekani, Michael Clarke Duncan amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 54.

Duncan aliwahi kuigiza kwenye filamu nyingi zikiwemo “Friday”, “The Green Mile”, na “The Whole Nine Yards.”

Kwa mujibu wa vyanzo, muigizaji huyo amefariki ghafla.

Mtandao wa TMZ umesema kuwa mchumba wake Omarosa Manigault alikuwa naye kwenye hospitali jijini Los Angeles na kuondoka kwa kipindi kifupi. Aliporudi alimkuta mpenzi wake ameshafariki.

Vyanzo hivyo vimesema kuwa mama yake Omarosa alikuwa naye wakati akiaga dunia.

Pamoja na kuwa muigizaji Duncan aliwahi kufanya kazi kama bodyguard wa watu maarufu wakiwemo Will Smith, Martin Lawrence, Jamie Foxx, LL Cool J, na Notorious B.I.G. kabla ya kuacha kazi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents