Michezo

Wayne Rooney ammwagia sifa beki Chris Smalling na Anthony Martial

Nahodha wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amesema beki Chris Smalling kwa sasa ni miongoni mwa walinzi watatu bora wa kati duniani.

2DC4587500000578-3290068-image-a-5_1445869566416

Alisema hayo wakati akizungumza na mtandao wa klabu wa Manchester United alipoulizwa kuhusu uwezo wa Chris Smalling msimu huu. Rooney alisema anakubali kupanda kwa kiwango cha mlinzi huyo msimu huu huku akimtaka aendelee kuwa kiongozi katika safu ya ulinzi.

“Chris ni miongoni mwa mabeki wakati bora hivi sasa. Ni miongoni mwa mabeki bora watatu wakati hivi sasa duniani,” alisema.

Hivi karibuni kocha Louis Van Gaal alimmwagia sifa pia Chris Smalling kwakuwa na uwezo mkubwa kikosini hivi sasa huku akisema siku moja atakuja kuchukua mikoba ya unahodha wa Manchester United baada ya Rooney na Carrick kuondoka.

Smalling anatajwa kuwa ndiye mchezaji aliye-perform katika kiwango cha juu msimu huu katika kikosi cha Louis Van Gaal.

Anthony.jpg 2

Rooney pia alimmwagia sifa kijana chipukizi Anthony Martial ambaye kabla ya kujiunga na Man United alikuwa hamfahamu lakini alipojiunga na timu hiyo ameona uwezo wake msimu huu akitokea Monaco. Amesema kuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini hivi sasa na kwamba atawasaidia kupata chochote msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents