Burudani

Adele akiri kuwa mtoto wake si shabiki wa muziki wake

Licha ya muziki wake kupendwa na idadi kubwa ya mashabiki mbalimbali duniani, mwanamuziki wa Uingereza, Adele amekiri kuwa mtoto wake wa kiume si shabiki wa muziki wake.

Adele2

Akiwa kwenye mahojiano na BBC Radio 2, Adele aliulizwa kama huwa anamwimbia mtoto wake wa miaka mitatu aitwaye Angelo, alijibu kuwa hua anamwiambia lakini hapendi nyimbo zake.

Mshindi huyo wa Grammy ambaye ameachia wimbo mpya ‘Hello’ baada ya ukimya wa miaka minne, pia alielezea jinsi ambavyo huwa anapatwa woga kila anapopanda jukwaani.

“I do really love performing but I can’t get over my nerves, I don’t really enjoy it until I’m off stage.” Alisema Adele.

Video ya Adele ambayo ilivunja rekodi ya YuoTube kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 25 siku ya kwanza, hadi sasa ina views milioni 84.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents