Michezo

Wayne Rooney kuwa nje kwa mwezi mzima

Nahodha na mshambuliaji Man United, Wayne Rooney atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima baada ya kuumia.

article-3451663-3153C13500000578-683_636x382

Kuumia kwa Rooney ni hofu kwa Kocha Louis van Gaal wa Man United, na Kocha Mkuu wa England, Roy Hodgson.

Taarifa zinasema ameumia goti katika mechi dhidi ya Sunderland na vipimo vimeonyesha kuwa anahitaji matibabu.

Manchester United imesafiri kwenda Denmark kucheza na Midtjylland katika mechi ya michuano ya Europa Cup. na imeondoka bila ya Rooney.

Van Gaal amethibitisha hilo na kusema wanaendelea kusubiri ili kupata uhakika.

Taarifa kutoka katika gazeti la The Guardian la England, zinaeleza Rooney atakaa nje kwa mwezi mzima.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents