Mitindo

Asia Idarous asema alikuwa sekretari kabla ya kuingia kwenye ‘Fashion’ ambayo imebadili maisha yake

Mbunifu mkongwe wa mavazi, Asia Idarous amefunguka na kueleza jinsi alivyoweza kubadili maisha yake kutoka kuwa sekretari wa ofisi hadi kwenye fani ya ubunifu wa mavazi ambayo imebadili maisha yake.
1

Akizungumza na BBC Swahili Jumatano hii, Asia alisema haikuwa rahisi kupata mafanikio aliyonayo sasa.

“Nilikuwa sekretani wa ofisi mwanzoni,” alisema Asia.

“Nilikuwa tayari ni fashion designer lakini mdogo mdogo. Kwahiyo kusema kweli nimeendelea na kazi yangu baada ya kuchukua diploma. Mpaka leo hii nikikwambia ni kazi ambayo inaniendeshea maisha yangu, nasomesha watoto wangu. Unapofanya kazi uwe na malengo kwamba kazi yako, unaitegemea kiasi gani na ufanyeje ili uweze kupata kipato ambacho kitaendesha maisha yako,” aliongeza.

Pia mwanamitindo huyo ambaye ni mwanzilishi wa onyesho la ‘Kanga za Kale’, ameeleza njia mbalimbali ambazo zitawasaidia wabunifu wachanga kufikia malengo yao.

“Katika kazi yoyote usiwe mbinafsi, na pili fanya kazi zako kwa heshima kila mtu atakuthamini na atakufuata. Onyesha mapenzi kwa wenzio, ukiona una nafasi ya kuwasaidia wengine wape nafasi. Pia ujitaidi kubuni vitu vyako, usiige vitu vya watu.,” alisema Asia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents