Promotion

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao aanza ziara maalum ya kutembelea vyombo vya habari nchini

001.TOUR
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) akishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio one, Joyce Mhavile ( kulia)akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia ( kushoto) wakati uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea kituo cha ITV na Redio One jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuelendeleza Mahusiano mazuri ya kibiashara

002.TOUR
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhaville, (kulia) akiwafafanulia jambo wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kujifunza mbalimbali na kuelendeleza Mahusiano mazuri ya kibiashara,Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Meneja Uhusiano Matina Nkurlu,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia wakati uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea ITV na Redio One jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo

003.TOUR
Maofisa wa Vodacom Tanzania ,wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao(wapili kushoto) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Rosalynn Mworia (aliyekaa) Meneja Uhusiano Matina Nkurlu, (kushoto)na Meneja biashara,Grace Lyon wakioneshwa jinsi taarifa ya habari inavyoenda hewani na na mtangaziji wa kituo cha ITV Abdallah Mwaipaya

004.TOUR
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(wapili kulia) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ( kushoto) na Kaimu mkuu wa Masoko na Mawasiliano,Yvonne Maruma wakimsikliza kwa makini Mhariri wa ITV na Redio One,Stephen Chuwa alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na utendaji wa wa kituo hicho

005.TOUR
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhaville(kushoto) akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia

006.TOUR
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kushoto) akimsikiliza matangazaji wa kituo cha EATV, Deo alipoongoza Uongozi wa kampuni yake kutembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituni hapo jana
007.TOUR
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia , wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa East Africa Redio na EATV

008.TOUR
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Kampuni ya New habari Corporation jijini Dar es Salaam

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents