Habari

Wazazi waliomuita mtoto wao ‘Messiah’ huko Marekani waagizwa na mahakama kubadilisha jina hilo kwa madai kuwa ni la Yesu peke yake!

Alhamisi iliyopita hakimu wa Tennessee, Marekani aliwaagiza wazazi wa mtoto wa miezi saba kubadili jina la mtoto wao kutoka Messiah walilompa kwa madai kuwa jina hilo lilikuwa ni kwaajili ya Yesu kristo peke yake.

Messiah-1

Kwa mujibu wa ripoti ya WBIR wazazi hao ambao walimuita mwanao Messiah DeShawn Martin, walishindwa kukubaliana juu ya jina la mwisho hivyo wakaamua kwenda mahakamani kwaajili ya kupata msaada zaidi. Lakini bila kutarajia hakimu Lu Ann Ballew aliwaagiza kubadili jina la kwanza Messiah badala ya la mwisho, na kuwaambia wamuite Martin DeShawn McCullough linalojumuisha majina yote ya mama na baba.

Messiah-2

“The word Messiah is a title and it’s a title that has only been earned by one person and that one person is Jesus Christ,” Ballew aliiambia WBIR.

Messiah-3

Wazazi hao hawakuridhika na uamuzi huo hivyo wamepanga kukata rufaa kwaajili ya kumuita mwanao jina la Messiah.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents