Soka saa 24!

Wazazi washauriwa watoto wasilale na chuchu mdomoni, Madaktari wasema kuna madhara makubwa

Daktari bingwa wa afya ya kinywa na meno kwa watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Conrad Mselle  ameishauri jamii kuacha tabia ya kuwapeleka watoto kwa waganga wa jadi kwa madai ya kuwa na meno ya plastiki.

Pia ameshauri kutokumwacha mtoto alale na chuchu ya mama mdomoni hasa wakati wa usiku kwa kuwa bakteria wanaoishi mdomoni hutumia sukari kuzalisha tindikali inayosababisha meno kuvunjika.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Mselle alisema kitaalamu hakuna meno ya plastiki.

Wasiwapeleke kwa waganga wa jadi ambako wamekuwa waking’olewa kwa kutumia vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘spoku’ za baiskeli jambo linalosababisha kupata maambukizi mbalimbali,” alisema Dkt. Mselle.

Dkt. amesema wazazi wa watoto wenye changamoto yoyote ya kinywa wanatakiwa kuwapeleka kwa daktari wa kinywa na meno kwa uchunguzi na matibabu na si tiba mbadala.

Aidha alieleza kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwasababishia watoto madhara makubwa kiafya, ikiwa ni pamoja na kutokwa damu nyingi.

Dkt. Mselle alitolea mfano kuwa jamii nyingi za wafugaji wamekuwa wakitumia njia hiyo na kusababisha maumivu makali kwa watoto na hata wengine kupoteza maisha.

Niwashauri wazazi kusafisha vinywa vya watoto wao mara baada ya kuwapa dawa za maji (syrup) kwa kuwa kutokufanya hivyo bakteria huitumia kuzalisha tindikali na kuharibu meno,” alisema Dk. Mselle.

Chanzo: Gazeti Mtanzania

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW