Tupo Nawe

Waziri Mwakyembe amuomba Diamond avunje ratiba yake ya Wasafi Festival Iringa, Amtaka aweke utaifa mbele

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemuomba msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kubadilisha ratiba ya Wasafi Festival mkoani Iringa ili ahudhurie kwenye tamasha la kizalendo la JAMAFEST.

Akiongea na Waandishi wa Habari jana Septemba 19, 2019, Waziri Mwakyembe amesema kuwa tamasha la JAMAFEST (Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival) mwaka litafanyika katika Uwanja wa Taifa na litadumu kwa siku 8 na litahudhuriwa na wasanii wa ndani na nje ya Tanzania.

Akisisitizia uwepo wa Diamond, Waziri Mwakyembe amesema kuwa “Nimempigia simu kijana wetu nyota wa muziki barani Afrika na pia ulimwenguni ukipenda, Diamond kwamba sasa huu ndio muda wa kuonesha utaifa, hebu njoo ujiunge na sisi. Na atakuwa na ziara siku hiyo mkoani Iringa, Nimemwambia avunje ziara hiyo kwa utaifa, Nafikiri atafanya hivyo. Kwa sababu tulipokuwa Uganda wasanii wote wakubwa nchini humo walihudhuria kwenye tamasha“.

Kwa upande mwingine, Mwakyembe amewaomba Watanzania wahudhurie kwa wingi kwenye tamasha hilo, Wakiwemo wasanii wa Bongo Fleva ili kuonesha uwezo wao.

Tamasha la JAMAFEST litafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na linatarajiwa kuanza Wikiendi hii Septemba 22 hadi 28, 2019 katika Uwanja wa Taifa.

View this post on Instagram

BURUDANI: Waziri Mwakyembe amuomba Diamond avunje ratiba yake ya Wasafi Festival Iringa, Amtaka aweke utaifa mbele. ——————————————————————————- Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemuomba msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kubadilisha ratiba ya Wasafi Festival mkoani Iringa ili ahudhurie kwenye tamasha la kizalendo la JAMAFEST. Akiongea na Waandishi wa Habari jana Septemba 19, 2019, Waziri Mwakyembe amesema kuwa tamasha la JAMAFEST (Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival) mwaka litafanyika katika Uwanja wa Taifa na litadumu kwa siku 8 na litahudhuriwa na wasanii wa ndani na nje ya Tanzania. Akisisitizia uwepo wa Diamond, Waziri Mwakyembe amesema kuwa “Nimempigia simu kijana wetu nyota wa muziki barani Afrika na pia ulimwenguni ukipenda, Diamond kwamba sasa huu ndio muda wa kuonesha utaifa, hebu njoo ujiunge na sisi. Na atakuwa na ziara siku hiyo mkoani Iringa, Nimemwambia avunje ziara hiyo kwa utaifa, Nafikiri atafanya hivyo. Kwa sababu tulipokuwa Uganda wasanii wote wakubwa nchini humo walihudhuria kwenye tamasha“. . . . Kwa upande mwingine, Mwakyembe amewaomba Watanzania wahudhurie kwa wingi kwenye tamasha hilo, Wakiwemo wasanii wa Bongo Fleva ili kuonesha uwezo wao. Tamasha la JAMAFEST litafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na linatarajiwa kuanza Wikiendi hii Septemba 22 hadi 28, 2019 katika Uwanja wa Taifa. WRITTEN BY @mgallahtz , (Video Credit Mwanahalisi TV)

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW