Habari

Waziri Ummy awataka wanaume kutotumia likizo ya uzazi kunywea pombe 

Waziri Ummy awataka wanaume kutotumia likizo ya uzazi kunywea pombe 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wanaume kutoitumia likizo ya siku tano ya uzazi kwenda kunywa pombe.
Aidha, amesema ataifuta likizo hiyo kwa wanaume endapo atajiridhisha haina manufaa na inatumika ndivyo sivyo.
Akizungumza kuhusu Wiki ya Unyonyeshaji itakayoanza kesho hadi Agosti 8 mwaka huu, Waziri Ummy amesema likizo hiyo ni kwa ajili ya kumsaidia mama anapokuwa amejifungua na si vinginevyo.
“Likizo ya uzazi kwa wanaume si ya kwenda kunywa pombe, lakini wapo wanaume wanachukua likizo na nyumbani hawaonekani, nitafanya utafiti kuangalia iwapo ina manufaa kama hakuna tutaifuta,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents