Michezo

Wenger ampendekeza Arteta kuwa kocha mpya wa Arsenal

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema  kuwa Mikel Arteta anafaa kuwa mwalimu mpya wa timu hiyo kwakuwa anavigezo vyote vinavyohitajika.

Arteta amewahi kuwa nahodha wa Arsenal anakutimka baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka 22 kwa sasa anahusishwa kuhitaji kurithi mikoba ya Wenger.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 36, amecheza jumla ya michezo 150 ndani ya Arsenal na kwa sasa akiwa mwalimu ndani ya kikosi cha mabingwa wapya wa Uingereza Manchester City.

Alikuwa kiongozi, anahisia na mchezo, anafahamu tamaduni ya klabu na umuhimu wake. Arteta ambaye hajawahi kuwa kocha mkuu kwenye klabu yoyote amekuwa akijifunza kufanya hivyo ndani ya City chini ya meneja Pep Guardiola tangu mwaka 2016.

Naamini ni muhimu kufanya maamuzi yake binafsi na nitampa mchango wangu atakapo uhitaji, kwa vyote hivyo anasifa lakini sihitaji kumtangaza.

Hata hivyo amesema kuwa nivigumu kwake kufundisha timu nyingine za nchini Uingereza kutokana na muda wake aliyo utumia akiwa na Arsenal.

Ligi kuu nchini Uingereza ni mahala panapo vutia zaidi kuwepo, kuna uongoza tamaduni tofauti tofauti na hata mazingira yake huvutia pia.

Arsenal pia wana mawasiliano na nahodha mwingine ambaye ni Patrick Vieira ikiwa ni sehemu ya wanao wania kurithi mikoba ya Wenger. Hata hivyo bado ni siri nani atakuwa kocha mpya wa ndani ya klabu hiyo na kutangazwa Juni 14 klaba ya kuanza kwa kombe la Dunia nchini Urusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents