Michezo

West Ham kumrudisha Patrice Evra Uingereza

Klabu ya West Ham inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ipo katika mikakati ya kumsajili beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra.

Evra mwenye umri wa miaka 36, atajiunga na West Ham akiwa kama mchezaji huru baada ya kuachwa na klabu ya Marseille kufuatia kumpiga shabiki wa timu hiyo na UEFA kumpatia adhabu.

Patrice Evra aliwasili kwa wagonga nyundo hao wa jiji la London hapo jana siku ya Jumanne na kufanya mazoezi katika  kiwanja cha timu hiyo ikiwa ni ishara ya kurejea ligi ya Uingereza.

Kufuatia kitendo cha beki huyo kumpiga teke shabiki UEFA ilimuadhibu kutoshiriki mashindano ya barani Ulaya hadi mwezi Juni na faini ya pauni 9,000.

Kitendo alichofanya Evra kinakumbusha tukio la Eric Cantona dhidi ya shabiki wa Crystal Palace mwaka 1995.

Evra ameshiriki michezo 300 akiwa  United kabla ya kuondoka msimu wa mwaka 2013/14 chini ya Moyes.

Beki huyo ametwaa mataji matano ya ligi ya Uingereza akiwa  Old Trafford pamoja na taji moja la Champions League kabla ya kuelekea Italia ambako alitwaa mataji mawili ya  Serie A na Coppa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents