Habari

Winnie Mandela mke wa zamani wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini amtembelea mzee Nelson Mandela hospitali alipolazwa siku nne sasa!

Rais wa zamani wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini huko Pretoria Afrika Kusini ikiwa ni siku ya nne sasa kutokana na matatizo ya mapafu. Mandela ambaye amelazwa mara nne ndani ya miezi 6 ametembelewa na aliyewahi kuwa mke wake Winnie Mandela.

Mandela

Winnie Mandela mwenye miaka 76, alifika hospitalini hapo jana (June 10) ambapo alitumia muda wa takribani saa moja pembeni mwa kitanda cha mzee Mandela pamoja na wanafamilia wengine.

winnie-1

Winnie-2

Kwa mujibu wa BBC Swahili, taarifa kutoka ofisi ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini zinasema mzee Mandela ambaye mwezi ujao (July) atakuwa anatimiza miaka 95 , alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi toka Jumamosi alipofikishwa hospitalini hapo na pamoja kuwa hali yake ni mbaya lakini imeweza kudhibitiwa.

Aidha, mke wa sasa wa mzee Madiba Graca Machel aliyekuwa ziarani nchini Uingereza, alilazimika kuahirisha ziara yake na kurejea Afrika Kusini Jumamosi kwaajili ya kuwa na mume wake katika kipindi hiki cha ugonjwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents