Burudani

Wizkid apata shavu kutoka kwa rapper Future

Milango ya neema inazidi kufunguka kwa Wizkid. Msanii huyo kutoka Nigeria amepata shavu la kuwa miongoni mwa wasanii watakao tumbuiza kwenye show za ziara ya rapper Future ‘The Future Hndrxx Tour’ kutoka Marekani.

Katika ziara hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kuwaka moto Julai 8 ya mwaka huu, Wiz anatumbuiza katika show nne. Show ambazo Wizkid atawasha moto ni pamoja na itakayo fanyika West Palm Beach, Atlantic City, Syracuse na Uncasville (zote za nchini Marekani).

Kupitia mtandao wa Instagram, Wiz amethibitisha hilo kwa kuweka cover ya show zake atakazofanya na kuandika, “Catch me on the road with @future !! Bringing that African wave! ??? #starboyworldwide #freebandz.”

Ziara hiyo ya Future itazunguka karibia nchi kibao duniani ikiwemo kwenye bara la Marekani, Ulaya, Afrika na mengine. Ratiba hiyo pia imeonyesha rapper huyo wa Marekani atatumbuiza katika jiji la Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Leaders Julai 22.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents