Habari

Shirika la Hali ya Hewa duniani laja na mpango wa kuunusuru Mlima Kilimanjaro

Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO), limekubali kuuingiza Mlima Kilimanjaro kwenye Program yake inayoshughulika na nchi zenye barafu ulimwenguni ili kuunusuru na janga la kuyeyuka kwa barafu .

Tokeo la picha la mount kilimanjaro

Akizungumza na Wataalamu wa shirika hilo waliokutana jana jijini Arusha Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini, Dkt. Agness Kijazi amesema hiyo ni hatua ya msingi itakayotoa fursa kwa wataalamu wa hali ya hewa kufanya tafiti mbalimbali ili kubaini chanzo cha kupungua kwa barafu ya mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.

Kwa upande mwingine Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hatua hiyo pia itakuwa fursa kwa wataalamu kufanya utafiti kwenye maeneo mengine yenye barafu nchini Tanzania.

Nchi nyingine ya ukanda wa Afrika Mashariki inayotajwa kuwa na eneo lenye barafu ni nchi ya Kenya kupitia mlima Kenya.

Chanzo:ITV

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents