BurudaniHabari

RC Makonda Kuurasmisha Mchezo wa Pikipiki Arusha (Video)

Mimi ni maskini mwenzenu – RC Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, @baba_keagan leo, Jumapili Aprili 28.2024 amekutana kwa ajili ya mazungumzo na kikundi cha vijana wanaojihusha na mchezo wa kuendesha Pikipiki Arusha ambapo amewapongeza kwa kazi wanayoifanya hata hivyo ametoa wito kwa vijana hao kuendelea kuamini katika ndoto zao, na kwamba kupitia mchezo huo wanapaswa kutimiza ndoto hizo

Katika kuhakikisha ndoto za vijana hao zinatimia Makonda amewataka kuunda uongozi haraka iwezekanavyo, ambapo pamoja na mambo mengine uongozi huo utashirikiana na ofisi yake (ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha) katika kuandaa mipango ya kuhakikisha mchezo huo unatangazwa kama sehemu ya kivutio cha Arusha, hiyo ikienda sambamba na wachezaji wake kunufaika kwa kujipatia kipato kitakachoweza kuendesha maisha yao kama ilivyo kwa wanamichezo wengine

Amesema miongoni mwa mambo anayokusudia kufanya ni pamoja na kuandaa mashindano maalumu ambayo licha ya kwamba mashindano hayo yatatafutiwa wadhamini lakini ofisi yake kwanza inakusudia kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 kwa mshidi wa kwanza, milioni saba (7) kwa aliyeshika nafasi ya pili na shilingi milioni tano (5) kwa mtu wa tatu, kiasi ambacho kinaweza kuongezeka kutokana na idadi ya wadhamini watakojitokeza na kiasi cha pesa watakachotoa.

Kuangalia Video kamili bonyeza link hapa chini:

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents