Habari

Wyclef Jean awasili Lagos, tayari ku-host show ya ‘Rythm Unplugged 2013’ ambayo Vanessa Mdee pia atatumbuiza

Vanessa Mdee aka Vee Monoey ndiye msanii pekee wa Tanzania ambaye amepata nafasi ya kutumbuiza katika show kubwa nchini Nigeria ya ‘Rythm Unplugged 2013’ ambayo inatarajiwa kufanyika kesho na host wa show hiyo atakuwa msanii wa Marekani Wyclef Jean.

Wyclef Jean in nigeria
Wyclef baada ya kuwasili Naija

Wyclef Jean tayari amewasili nchini humo kwa ajili ya show hiyo kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na kuhusisha wasanii wakubwa wa Naija wakiwemo P-Square, Wiz Kid, Davido, D’Banj na wengine.

Wyclef Jean in lagos

Jean alitweet masaa machache kabla hajaondoka Marekani,
“I am on my way to Africa today !v “Nigeria” “Ghana” We all Love Nelson Mandela! Then I will be in Jamaica my second home performing at “sting”.

Hii ni mara ya pili kwa Wyclef kwenda Nigeria kuhost tamasha la muziki, baada ya ile ya MTV Africa Music Awards.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents