Tia Kitu. Pata Vituuz!

Yafahamu mataifa matano yenye kesi nyingi zaidi za wagonjwa wa Corona na jumla ya waathirika wote duniani, Afrika Misri yaongoza

Yafahamu mataifa matano yenye kesi nyingi zaidi za wagonjwa wa Corona na jumla ya waathirika wote duniani, Afrika Misri yaongoza

Kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyoendelea kusambaa kote duniani ambapo yalianzia katika taifa la China na sasa virusi hivi vimetapakaa karibia dunia nzima kwani katika kila bara kwa sasa kuna maambukizi ya corona.

Ikiwa China ndio nchi ya kwanza kuvivumbua virusi hivyo na kwa sasa ikiwa na kesi za Corona takribani 80881 huku wanaokadiriwa kupona wakiwa ni 61644 na walipoteza maisha wakiwa ni 3226.

China wakifuatiwa na taifa la Italia lenye kesi 27980 waliopona wakiwa 1045 na walipoteza maisha wakiwa ni 2158.

Taifa la 3 kwa kuwa na kesi nyingi za Corona likiwa ni Irani lenye kesi 14 991 walipona wakiwa ni 2959 na walipoteza maisha wakiwa ni 853.

Taifa la 4 ni Uhispania lenye kesi za Corona zipatazo 99422 huku waliopona wakiwa ni 183 na waliopoteza maisha wakiwa ni 342.

Taifa la 5 likiwa ni Korea Kusini likiwa na kesi za Corona 8320 huku waliofanikiwa kupona ikiwa hakuna hata mmoja na walipoteza maisha wakiwa ni 75 mataifa yanayofuata yakiwa ni Ujerumani waathirika 7272 waliopona wakiwa 25 na walipoteza maisha ni 17, Ufaransa kesi 6633 waliopona 1 na walipoteza maisha 148, Marekani wakiwa na kesi 4667 walipona ni 8 na walipoteza maisha wakiwa 87.

Kwa upande wa bara la Afrika taifa linaloongoza kwa kuwa na kesi nyingi za Corona likiwa ni Misri lenye kesi166 huku waliopoteza maisha wakiwa ni 4 na walipona wakiwa 27, Misri inafuatiwa na taifa la Afrika Kusini lenye kesi 64 huku mpaka hivi sasa hakuna aliyepona wala aliyepoteza maisha taifa la 3 ni Algeria lenye kesi 60 na walipoteza maisha wakiwa 4 na mpaka hivi sasa kukiwa hakuna aliyepona hata mmoja. taifa la Morocco likiwa na kesi 38 waliopona 3 na hakuna aliyepoteza maisha, Senegal kesi zikiwa 6 huku aliyepona akiwa mmoja na hakuna aliyepoteza maisha.

Hayo ni mataifa yanayoongoza kwa kuwa na kesi nyingi za virusi vya Corona lakini pia mataifa ya Afrika yanayoongoza kwa kuwa na kesi nyingi za Corona na mpaka hivi sasa jumla ya kesi za waathirika wa kesi za Corona duniani kote ni 182550 na waliofanikiwa kupona duniani kote wakiwa ni 67003 na walipoteza maisha wakiwa ni 7158.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW