Michezo

Yanga kuwakosa wachezaji wanne kikosi cha kwanza kombe la shirikisho

Klabu ya soka ya Yanga ambayo Jumamosi hii inatarajiwa kucheza na Welayta Dicha ya Ethiopia katika kombe la shirikisho barani Afrika, itawakosa wachezaji wake wanne muhimu.

Wachezaji hao ambao wataukosa mchezo huo ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Said Makapu.

Wachezaji hao wataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi nyingi za njano ambazo walipata kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika.

Wapinzani hao wa Yanga wanatarajiwa kuwasili mchana wa leo (Jumatano) kwenye uwanja wa ndege wa Mwl. JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents