Michezo

Yanga SC waeleza kuhusu jina la Youthe Rostand kutumwa CAF

Wakati klabu kongwe zaidi ligi kuu soka Tanzania Bara, Dar es Salaam Young Africans ikiingia mazoezini hii leo kujiweka sawa tayari kuvaa timu ya St Louis katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika, meneja wa kikosi hicho, Hafidhi Saleh amesema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa ya jina la mlinda lango wao, Youthe Rostand kutopelekwa Caf.

Hafidh ameyasema hayo kupitia tovuti ya klabu hiyo wakati huu ambapo kumezuka tetesi za jina la Riostand kiutopelekwa Caf.

“Ni uzushi tu usikuwa na maana, jina la Rostand lilitumwa CAF na leseni yake ya kucheza mashindano ya klabu bingwa tunayo, hivyo siyo kweli kwamba jina lake halikutumwa, kuhusu kucheza au kutokucheza mchezo siku zote benchi la ufundi ndiyo hupanga kulingana na mipango ya mchezo husika,”amesema Hafid.

Mapema mwanzoni mwa wiki hii mabingwa hao watetezi walifanikiwa kuchomoza na pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Majimaji na hivyo kupunguza pengo lililopo dhidi ya vinara wa ligi Simba SC ambayo jana ililazimishwa sare ya goli 2-2 na Mwadui FC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents