Michezo

Yanga yapewa msaada na TFF ili iweze kurudi nyumbani

Wachezaji wa klabu ya Yanga sasa wanatarajia kuingia Dar es Salaam leo kutoka nchini Algeria.

Wameondoka na ndege ya Emirates badala ya Turkish Airways na imeelezwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limelazimika kutoa mkopo kwa klabu hiyo ili kuwakomboa.

Wachezaji saba na katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa walichelewa ndege jijini Algeria na kulazimika kusubiri hadi Jumanne ndiyo waondoke na kutua nchini siku ya jumatano.

Wachezaji walioachwa ni Kelvin Yondani, Deogratius Munishi ‘Dida’, Emanuel Martin, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Haruna Niyonzima, Endrew Vicent ‘Dante’ Juma Abdul, Mwinyi Haji, Deus Kaseke, Ben Kakolanya pamoja na Mkwasa mwenyewe.

Mkwasa alisema wataomba msaada kwa MC Alger waliokwenda kucheza nao na kufungwa mabao 4-0 kwa kuwa hawakuwa na fedha za kutosha.

Lakini msaada huo wa TFF utawafanya warejee haraka nyumbani na si Jumatano tena kama ambavyo ilikuwa ikitarajiwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents