Michezo

Yanga yavuliwa ubingwa rasmi jijini Mbeya

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imekubali kipigo cha mabao 2 – 0 dhidi ya TZ Prisons kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Kukubali kipigo cha mabao hayo 2 – 0 dhidi ya TZ Prisons kinaifanya Yanga kuvuliwa ubingwa rasmi wa ligi kuu Tanzania Bara.

Yanga yenye pointi 48 ilihitaji kushinda michezo yote sita huku akiiyombea dua baya hasimu wake Simba kupoteza walau mechi moja ili kujihakikishia kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo lakini hali imekuwa tofauti hii leo baada ya kukubali kipigo hicho mbele ya Prisons.

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba mpaka sasa inajumla ya pointi 65 huku ikisaliwa na michezo mitatu mkononi kabla ya kumaliza msimu huu wa mwaka 2017/18.

Waliopeleka kilio mitaa ya Jangwani hii leo ni wachezaji, Eliuter Mpepo katika dakika ya 58 na Salum Bosco kunako dakika ya 85 ya mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents