DStv Inogilee!

Young Dee: Nimejifunza jinsi ya kudeal na skendo bila kuathiri kazi yangu

Kuna baadhi ya wasanii ambao hutengeneza skendo kwa lengo la kufanya wazungumziwe zaidi ili kusaidia kwenye muziki wao, lakini wapo wengine ambao hujikuta wakihusishwa na skendo za uongo ambazo huwaathiri kwa namna moja ama nyingine.

young-Dee

Young Dee ni miongoni mwa wasanii ambao wamewahi kuhusishwa kwenye skendo mbalimbali, lakini kubwa ambayo hata yeye mwenyewe amekiri imekuwa ikimsumbua ni ile ya kudaiwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya, jambo ambalo amelikanusha mara kibao akisema kubwia unga ni jambo lisilofichika kwahiyo kama ni Kweli ingejidhihirisha.

Akizungumza kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Young D amesikika akisema msanii asipokuwa makini anaweza kujikuta anatumia muda wake mwingi kufikiria skendo ambazo muda mwingine hazina ukweli.

Dee ameongeza kuwa yeye binafsi ameshazoea issue hizo kwa hiyo amejifunza jinsi ya kudeal nazo bila kuathiri kazi yake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW