Habari

YouTube Music Awards : YouTube kuanzisha tuzo zake za muziki mwaka huu

Mtandao wa YouTube umetangaza kuanzisha tuzo zake za muziki ‘Youtube Music Awards’ zitakazokuwa zikitolewa kwa wasanii waliofanya vizuri katika miaka ya karibuni.

youtube

Kwa mujibu wa blog rasmi ya Youtube, Mkali wa flow ambae pia ni producer Marshall Bruce Mathers III aka ‘ Slim Shady, Eminem’ na Lady Gaga ni miongoni mwa wasanii ambao watatumbuiza katika uzinduzi wa tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza (Novermber 3) mwaka huu jijini New York, Marekani.

Eminen atapanda katika jukwaa hilo ikiwa ni siku mbili tu kabla hajaachia rasmi album yake inayosubiriwa kwa hamu ‘Marshal Mathers LP2’ itakayoingia sokoni November 5, huku wimbo wake ‘Berzerk’ unaopatikana kwenye album hiyo ukiendea kufanya vizuri kwenye media.

Katika uzinduzi/ufunguaji wa Tuzo hizo ambazo hazijawahi kutolewa, itapewa heshima video itayokuwa imeangaliwa zaidi kwenye Youtube ambapo uchaguzi utazingatia jinsi ilivyoangaliwa kwa mtazamo wa dunia nzima (global music- video views) na kushare.

Creative Director wa show za tuzo hizo Filmaker Spike Jonze, ameahidi kuwa tukio hilo litakuwa la aina yake. Majina ya watakaowania tuzo hizo (Nominations) yatatajwa October 17 mwaka huu na watu wataweza kupiga kura zao kupitia mitandao ya kijamii.

Tukio la ugawaji wa tuzo hizo litaoneshwa live kwenye mtandao kutoka New York.

SOURCE: YOUTUBE OFFICIAL BLOG

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents