Michezo

Zlatan na Pogba kuikabili Newcastle

Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wanatarajiwa kurejea dimbani siku ya Jumamosi kuikabili Newcastle huko Old Trafford.

 

Ibrahimovic  mwenye umri wa miaka 36 amekuwa nje ya uwanja tangu apate majeraha mwezi Aprili.

Wakati kiungo wa timu hiyo Pogba mwenye umri wa miaka 24 hajacheza mchezo wowote tangu apate majeraha wakati timu yake ilipoikabili klabu ya Basel mwezi Septemba.

Huku mchezaji, Marcos Rojo pia akitarajiwa kuwepo na meneja wa kikosi cha United, Jose Mourinho akisisitiza kuwa wote amewapanga.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Sweden, Ibrahimovic huu utakuwa mchezo wake wa 46, huku akiwa amefunga jumla ya mabao 28 ndani ya United msimu uliyopita.

Mourinho amesema Romelu Lukaku atakuwa sambamba na Ibrahimovic hapo kesho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents