Burudani

​Rama Dee aeleza sababu ya wimbo wake Kipenda Roho kuwa na video nyingi

Muimbaji wa RnB, Rama Dee amesema wimbo wake Kipenda Roho una video nyingi kwasababu ni hadithi ambayo inaweza kuwasilishwa kwa namna nyingi. 

Hivi karibuni ataachia video nyingine ya wimbo huo iliyoongozwa na Adam Juma.
Amesema nia yake ni kuwapa nafasi waongozaji mbalimbali kufanya video ya wimbo huo kwa ubunifu wao wenyewe.
“Nimetoa ruhusa kwahiyo inawezekana Hanscana naye akaja akafanya na wengine,” amesema.
Amesema wapo wengine wameshafanya video zao na wamemtumia na atakuwa akizitoa huku akiweka milango wazi kwa wengine pia.
Sababu nyingine amesema ni kurudisha imani kwa waongozaji wa video wa nyumbani na kuwalipa vizuri.
“Sisi watanzania tujivunie katika upande wote, wa video, directors na kila kitu ambacho kipo. Tuipaishe Tanzania kwa nguvu zote. Huwezi kusema unaenda kutamba Nigeria wakati una video ya Nigeria na style ya Nigeria. Wapo wanakusupport sababu unasupport style yao,” amesisitiza Rama Dee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents