Habari

Tanzania yatoka tena mikono mitupu Olimpiki

Jana michuano ya Olimpiki imefungwa rasmi jijini London Uingereza na kuifanya Tanzania kutoka mikono mitupu kwa mwaka wa 40 mfululizo.
Katika mbio za marathon mwanariadha wa Tanzania Faustine Musa alijikuta akishika nafasi ya 33 na mwenzie Samson Ramadhan kushika nafasi ya 66.
Michuano hiyo imeshuhudia timu ya Tanzania ikigeuka watalii wa jijini London kama kawaida wakati wanamichezo wa Kenya na Uganda wakiwatoa kimasomaso wananchi wake.
Uganda imetoka na medali moja ya dhahabu na Kenya kuchukua medali mbili za dhahabu, nne za fedha na tano za shaba.
Marekani ndio inayoongoza kwa kuwa na medali nyingi zaidi kwa kunyakua medali 46 za dhahabu ikifuatiwa na China yenye medali za dhahabu 38.
Wenyeji wa michuano hiyo Uingereza, imekamata nafasi ya tatu kwa kushinda medali 29 za dhahabu, matokeo bora zaidi tangu miaka 104 iliyopita.
Nafasi ya nne imekatwa na Urusi kwa kunyakua medali 24 za dhahabu ikifuatiwa na Korea yenye medali 13.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents